Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja amewahakikishia wasambazaji bidhaa na wanaodai kwamba utawala wake utalipa polepole deni la kaunti la Sh bilioni 86. Sakaja alisema deni hilo limeongezeka kwa miongo kadhaa, kuanzia Baraza la Jiji la Nairobi la zamani na Huduma za Jiji la Nairobi zilizofutwa. Alisema mrundikano wa awali ulikuwa umezidi Sh bilioni 109 lakini ulipunguzwa kupitia ukaguzi, mapitio ya madai na mazungumzo.

JOHNSON SAKAJA - OWED