Mwanamume mmoja kutoka Isiolo amehukumiwa kifungo cha miaka 25 gerezani kwa kumnajisi  mtoto wa miaka 15 mwenye ulemavu wa akili. Mwanamume huyo alipatikana na hatia baada ya upande wa mashtaka kuwasilisha ushahidi kutoka kwa mtoto huyo, mashahidi wengine watano, pamoja na ushahidi wa kimatibabu. Mahakama iliona kuwa ushahidi huo ulikuwa wa kutosha kuthibitisha kosa hilo pasipo shaka yoyote. Mfungwa huyo ana muda wa siku 14 kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.