Mahakama Kuu inatarajiwa kutoa uamuzi wake wa mwisho kuhusu ombi la Seneta wa Busia, Okiya Omtatah, linalopinga utaratibu wa kujumlisha matokeo ya kura za urais katika ngazi ya kitaifa. Omtatah anapinga kuanzishwa na kuendeshwa kwa kituo cha kitaifa cha kujumlisha matokeo, akisisitiza kuwa Katiba inaweka jukumu la msingi na la mwisho la kujumlisha, kuhakiki na kutangaza matokeo ya urais katika ngazi ya eneo bunge. Seneta huyo anataka mahakama itamke kuwa mchakato wa kujumlisha matokeo kitaifa ni kinyume cha Katiba na kuizuia IEBC kujumlisha au kuhakiki upya matokeo ya urais baada ya kutangazwa na maafisa wanaosimamia uchaguzi katika maeneo bunge.