Chama cha walimu KUPPET kimewatetea wakuu wa shule wanaopeleka fedha kwa muungano wa walimu wakuu wa shule za upili, ikisema kuwa fedha hizo huchangia katika shughuli za ziada za mtaala. Katibu Mkuu wa KUPPET, Akelo Misori, anasema kuwa ruzuku iliyotengwa kwa ajili ya shughuli hizo haitoshi, jambo linalozilazimu shule kutegemea fedha za ziada. Anasema KESSHA ina jukumu muhimu katika kuratibu shughuli hizo na inapaswa kutambuliwa na Wizara ya Elimu kama mdau muhimu.

AKELO MISORI - CO-CURRICULAR