Utofauti wa Kenya unapaswa kutumiwa kama chanzo cha nguvu na umoja wa kitaifa, badala ya kuonekana kama kikwazo cha maendeleo; haya yamesemwa na Katibu wa Utawala katika Ofisi ya Rais, Peter Mbugi. Akizungumza katika mkutano wa wadau kuhusu utofauti, ushirikishwaji na haki za watu wenye ulemavu, Mbugi alisema kuwa ingawa watu wanaweza kutofautiana katika asili, jamii na hali zao za maisha, wanaendelea kuwa na umoja kupitia nchi moja na matarajio ya pamoja ya kitaifa.
PETER MBUGI - IDENTITY