Wanaharakati huko Taita Taveta wanazitaka jamii kuwaunga mkono wasichana waliopata ujauzito wakiwa shuleni ili warejee darasani. Mwanaharakati Jeniffer Mwandawiro amezihimiza serikali ya kitaifa na ile ya kaunti kuhakikisha kuwa sera ya kuruhusu wanafunzi kurejea shuleni inatekelezwa mashinani, jambo litakalowawezesha akina mama hao vijana kujenga upya maisha yao kupitia elimu. Mwandawiro anasema kuwa takriban wasichana 2,000 walipata mimba katika Kaunti ya Taita Taveta mwaka uliopita.
JENIFFER MWANANDAWIRO - SHULENI