Mbunge wa Mwala na Katibu wa Kitaifa wa Uratibu wa chama cha UDA, Vincent Kawaya, amewaalika Mbunge wa Embakasi East, Babu Owino, na wanachama wengine wa vuguvugu la 'Linda Mwananchi' kujiunga na chama tawala cha UDA, kufuatia ripoti za kuwepo kwa migogoro ndani ya vuguvugu hilo. Kawaya alisema kuwa UDA ina ajenda ya wazi ya maendeleo na ruwaza ya muda mrefu, huku akiwahimiza viongozi ambao hawajaridhishwa na mwelekeo wa 'Linda Mwananchi' kuzingatia uwezekano wa kujiunga na chama hicho tawala.


VINCENT KAWAYA – LINDA MWANANCHI