Manchester United walisalimisha uongozi wa 2-0 na kutolewa nje ya kombe la ligi kufuatia kupoteza 3-2 mikononi mwa Brighton huko Old Trafford jana usiku. Shea Lacey na Mason Mount waliiweka United mbele kwa mabao mawili ya haraka dakika ya 8 na 10, kabla ya Charalampos Kostoula kupata bao moja kabla ya mapumziko. Pascal Grobb na De Cuyper walifunga katika kipindi cha pili kukamilisha marejeo. Wakati huo huo, Tami Abraham alifunga mabao mawili, huku Aston Villa ikiishinda Coventry 3-1, Everton ikiishinda Wolves 1-0 na Fleetwood ikiibandua Sheffield United.


 

Barclona ilifungua tena pengo la pointi tatu kileleni mwa La liga kwa kuichapa Racing Santander 7-2 jana usiku kwenye Uwanja wa Nou Camp. Raphinha aliendelea na mwanzo wake wa ajabu msimu huu kwa mabao matatu, huku bao la João Cancelo, Gabriel Jesus, Lamine Yamal na Asier Villalibre zikikamilisha aibu hiyo. Maguette Gueye na Yassir Zabiri walifunga mabao ya kufutia machozi kwa Santander waliopanda daraja. Wakati huo huo, Atletico iliishinda Osasuna 4-0 na Sevilla ikaishinda Deportivo iliyokuwa na wachezaji 10 bao 1-0.




Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Nairobi.

Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.