Jukwaa la Haki za Wanubi linatoa wito kwa serikali kurahisisha upatikanaji wa hati za utambulisho kwa watu kutoka jamii zilizotengwa. Akizungumza wakati wa hafla ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Utambulisho, Msaidizi wa Kisheria wa Uraia Rudhwan Haidar anasema waombaji bado wanakabiliwa na ugumu wa kupata vitambulisho vya kitaifa na vyeti vya kuzaliwa, licha ya serikali kufuta mchakato wa uhakiki. Anataka vikwazo vya kupata hati viondolewe.
RUDHWAN HAIDAR - ACESS