Seneta wa Kajiado, Seki Kanar, anataka ufafanuzi kuhusu kusitishwa kwa shughuli za uchimbaji madini na kampuni ya Tata Chemicals Magadi. Kanar anataka Kamati ya Seneti ya Mazingira ichunguze mkataba wa ukodishaji na mfumo wa kisheria wa kampuni hiyo, mazingira yaliyopelekea kusitishwa kwa shughuli hizo, malipo ya mrabaha, na iwapo kampuni imetimiza wajibu wake kwa wafanyakazi.

SEKI LENKU - MAGADI