Rais William Ruto anatarajiwa kuhudhuria kikao cha 81 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York, ambapo pia atakutana na Wakenya wanaoishi nchini Marekani. Katibu wa Wizara ya Mambo ya kigeni, Korir Sing’oei, anasema Rais atazindua Jukwaa la Kuimarisha Mchango wa Wakenya Wanaoishi Ughaibuni ili kuimarisha uhusiano kati ya serikali na Wakenya hao. Jukwaa hilo linatarajiwa kutoa fursa za uwekezaji na ushiriki wa Wakenya ughaibuni katika maendeleo ya Kenya.