Tume ya Kitaifa ya Jinsia na Usawa imezindua mijadala ya mashinani katika kaunti za Meru, Kisii na Nyamira ili kushughulikia vikwazo vinavyozuia ushiriki wa wanawake katika uongozi wa kisiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka uajo. Mijadala hiyo ya siku nne itashughulikia masuala ya ukatili wa kijinsia, mila na desturi zinazowapa wanaume mamlaka ya juu, uteuzi wa wagombea ndani ya vyama, ufadhili wa kampeni na changamoto za kitaasisi. Mwenyekiti wa tume hiyo, Rehema Jaldesa, alisema kuwa wanawake bado hawawakilishwi ipasavyo katika nyadhifa za uongozi zinazotokana na uchaguzi katika kaunti hizo tatu.