Waziri wa fedha John Mbadi anasisitiza kwamba pendekezo la kuuzwa kwa sehemu ya hisa za serikali za asilimia 15 katika kampuni ya Safaricom lilifuata utaratibu unaofaa. Akijibu uamuzi wa mahakama uliotangaza mchakato huo kuwa batili, Mbadi alisema uuzaji huo uliongozwa na usimamizi wa fedha wenye busara na hali halisi ya kifedha ya nchi. Alisema wizara yake inasoma uamuzi kamili ili kuandaa misingi ya kukata rufaa.
JOHN MBADI - CONFIDENT