Mgombea urais wa Jubilee Fred Matiang'i amemkosoa Rais William Ruto kwa kumuelezea Rais mstaafu Uhuru Kenyatta kama "kiongozi wa waasi" kuhusu madai ya ufadhili wa shughuli za upinzani kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2027. Matiang'i alisema Ruto anatumia muda mwingi kuwatafuta wafadhili wa upinzani badala ya kuwahudumia Wakenya waliomchagua. Alisisitiza kwamba kukosoa serikali na kushiriki katika shughuli halali za kisiasa ni sehemu ya mamlaka ya kidemokrasia ya upinzani na si uasi.