Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la haki za Wanubi Shaffie Hussein anasema kuendelea kuchunguzwa kwa waombaji wa vitambulisho na baadhi ya mashirika ya serikali kunanyima jamii zilizotengwa fursa muhimu. Hussein anasema baadhi ya waombaji wanalazimika kusubiri hati za vitambulisho licha ya tamko la rais la kukomesha desturi hiyo. Alizungumza Kibra wakati wa Siku ya Kimataifa ya Utambuzi, akitaka mchakato huo ufutwe kabisa.
SHAFFIE HUSSEIN - IDENTIFICATION