Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja amepatikana na hatia ya kuidharau mahakama kutokana na kuweka vizuizi vya barabarani wakati wa maandamano ya 'Gen Z' ya tarehe 25 Juni mwaka huu. Jaji Patricia Nyaundi jana alimwajibisha Kanja binafsi kwa vitendo vya maafisa wa polisi waliofunga barabara zinazoingia katikati ya jiji la Nairobi, licha ya agizo la mahakama lililowataka polisi kutoa taarifa ya awali kwa umma kabla ya kuweka vizuizi hivyo. Jaji alimwagiza Kanja kufika mbele ya Mahakama Kuu jumanne ijayo ili kutoa maelezo ya kujitetea kabla ya mahakama kuamua adhabu inayofaa kwa kosa hilo.