Biashara nchini Kenya zimehimizwa kutazama zaidi ya soko la ndani na kunufaika na fursa zinazoongezeka kote barani Afrika. Mtaalamu wa Biashara ya Kimataifa na Uchumi, Pauline Arunga, anasema ni muhimu kwa wafanyabiashara kufahamu ushuru, nyaraka zinazohitajika, viwango vya bidhaa za nje, gharama za usafirishaji na njia za malipo kabla ya kuingia katika masoko ya Afrika. Arunga anasema Uganda ndiyo soko kubwa zaidi la bidhaa za Kenya barani Afrika, huku thamani ya bidhaa zinazouzwa huko ikifikia takriban shilingi bilioni 163.