Wahariri wamehimizwa kuchukua jukumu muhimu katika kusaidia ustawi wa akili wa waandishi wa habari, haswa wanaposhughulikia kazi zenye kiwewe. Mwanasaikolojia Ruth Wangui amewahimiza waandishi wa habari pia kujifunza kuzungumzia hali ngumu na wenzao wanaowaamini na kutafuta tiba kutoka kwa washauri wa kitaalamu. Pia ametoa wito wa kujadiliana mara kwa mara kabla, wakati na baada ya kazi ngumu ili kuwasaidia waandishi wa habari kukabiliana na athari za kihisia za kazi zao.

RUTH WANGUI-SUPPORT