Barcelona bado ina matumaini ya kukamilisha usajili wa kiungo wa Manchester City Rodri. Hii ni licha ya kushindwa kwa dau la kwanza la takriban pauni milioni 42 kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania wiki iliyopita. Vyanzo vya klabu vinaonyesha kuwa ni mpango mgumu kuvuka mstari, lakini kuna matumaini kwamba watafanya hivyo baada ya tayari kukubaliana masharti binafsi na mshindi huyo wa kombe la dunia. City inamthamini Rodri kwa zaidi ya pauni milioni 60 huku Real Madrid pia ikiwa imeonyesha nia ya kumnunua mchezaji huyo wa zamani wa Atlético Madrid.
Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Kericho, Kitale na Kisii.
Ili kupata habari zaidi tembela tovuti ya radiojambo.