Serikali inasema ajali za barabarani huigharimu Kenya takriban asilimia tano ya Pato la Taifa kila mwaka kupitia gharama za huduma za afya, uzalishaji uliopotea na uharibifu wa mali. Akihutubia Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Usalama Barabarani, Mkurugenzi Mkuu wa NTSA Nashon Kondiwa alisema Kenya inakumbatia teknolojia, utekelezaji imara na kampeni za uhamasishaji kitaifa ili kupunguza vifo na majeraha ya barabarani.

NASHON KONDIWA – ROAD SAFETY