Mulamwah

SAA chache baada ya YouTuber Oga Obinna kudai kwamba alipatwa na mshangao kugundua mchekeshaji Mulamwah amemblock katika mitandao wa Instagram, Mulamwah ameibuka na kukiri kufanya hivyo, huku akitoa sababu.

Obinna Alifichua kulishwa block na Mulamwah wakati alipokuwa akijibu sababu ya kutotokea kusimama naye katika shoo yake binafsi ya kwanza iliyofanyika wikendi iliyopita.

Obinna alidai kwamba hakuwa na taarifa kuhusu kufanyika kwa shoo ya vichekesho ya Mulamwah na alipodokezewa, ndipo aliamua kumtafuta Instagram kuona lakini akapatwa na butwaa kugundua hawezi mfikia.

“Binafsi mimi sina bifu lolote na Mulamwah. Japo niligundua ile siku ya shoo yake kwamba ameniblock. Tulikuwa mjini nikaambiwa Mulamwah ako na shoo nikashtuka kuenda kuangalia nikapata niko blocked,” Obinna alieleza.

“Pia sikuwa najua kama shoo yake ilikuwa inafanyika ile siku kwa sababu ningeenda. Sababu kama nilikuwa sina shughuli mbona nisiende. Kwa wengine [ambao hawakuenda] siwezi jua. Lakini pengine walikuwa wameshikika, unaona siku kama za Jumamosi huwa na shughuli nyingi, angeweka kama Jumapili au Jumatatu labda wangetokea,” Obinna aliongeza.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Hata hivyo, Mulamwah alijitokeza na klipu ya Obinna akicheka wakati Dem wa FB alipokuwa anamueleza jinsi watu walikuwa wanamdhihaki mwanawe, Oyando Jr mitandaoni.

Katika klipu hiyo iliyochapishwa na Mulamwah kutoka kwa Weekly Show ya Obinna na Dem wa FB – kipindi ambacho kilifikia mwisho mwaka jana, alimkumbusha kwamba chanzo cha yeye kulishwa block kilitokana na hapo.

“Mwenye alienda haja kubwa njiani husahau lakini mwenye alikanyaga katu hawezi kusahau. Hapa ndipo ulikulia tofali,’ Mulamwah aliandika.

Kwenye klipu hiyo, Dem wa FB alikuwa anajaribu kumueleza Obinna jinsi watu walimkejeli mtoto wa Mulamwah mitandaoni, baadhi wakimfananisha na muigizaji marehemu Papa Shirandula.

Obinna alionekana kujaribu kuzuia kicheko chake kwa dhihaka hiyo, lakini inaonekana kujibeba kwake kwenye muktadha mzima kulimkera Mulamwah kufikia hatua ya kumblock.