HARMONIZE amekiri kwamba aliumia sana kuona baadhi ya Kauli mitandaoni zikimtuhumu babake kwa uchawi baada ya yeye kuondoka katika lebo ya Diamond Platnumz, WCB.
Kulingana na Mwanzilishi huyo wa Konde Gang, babake ni mtu wa dini sana na wala asingeweza kufikiria kuiendea WCB Wasafi kwa mganga ili kuiponza baada ya mwanawe kuota mbawa.
Harmonize Alifichua kwamba mmoja kati ya watu ambao waliumia sana alipoamua kuondoka kwa Diamond ni babake kwani muda wote alikuwa anawachukulia kama ndugu.
“Katika vitu ambavyo vilimuumiza sana babangu ni stori za mimi kuondoka WCB Wasafi. Mzee wangu unajua kama nilivyosema ni mtu wa dini japo umri wake kidogo umesonga. Alikuwa anatuchukulia mimi na Diamond kama watoto wake. Tulikuwa tuishi kama wasanii wa kufanya kazi pamoja muda wote,” Harmonize alieleza.
Alisisitiza kwamba hata yeye mwenyewe asingekubali ushawishi wowote wa kuiendea Wasafi kwa ushirikina, akitolea mfano wa jengo la msikiti nyumbani kwao ambao aliupa jina la Diamond.
“Ni kama mimi ninanavyoishi na Ibraah. Ndivyo ilivyokuwa kwa mimi na Diamond wakati huo. Kwa hiyo kusema mzee wangu anaweza akawa anashiriki kwa namna yoyote kutengeneza chochote kibaya kwa nia ya kuipoteza Wasafi sio kweli.”
“Mimi siamini hilo n anaweza kupa tu mfano kidogo. Mliona Masjid, Msikiti ambao naujenga kule nyumbani kwetu niliandika kwamba malipo ya kwanza ya kuanzisha ule msikiti alitoa Diamond.”
“Sasa wewe unawezaje kumfanyia uchawi mtu ambaye ametoa pesa yake ujenge msikiti kijijini kwako? Haileti maana,” alisema.
Hata hivyo, alionekana kutowalaumu waliozalisha uvumi huo akisema kwamba huenda ni kuchanganyikiwa kutokana na kutotarajia kwamba ukaribu wake na Diamond ungefikia mwisho.
“Ni kama kule kutengana kulikuwa kunamchanganya kila mtu kwamba inakuaje mbona hawa watu walikuwa washikaji sana.”
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!