Morgan Bahati//INSTAGRAM

MORGAN Bahati, mtoto wa kiasili wa msanii Bahati Kioko na Diana Marua amemshangaza mamake kwa kukiri kwamba amekuwa akitumia midomo yake kubusu.

Akizungumza na Diana Marua katika kipindi cha maswali na majibu kwenye Chaneli yake ya YouTube, Morgan alikiri kwamba amekuwa akibusu msichana mmoja tu lakini kwa mara kadhaa.

Tineja huyo alijitetea kwa hatua hiyo akitania kwamba midomo yake inapendeza mno kiasi kwamba hawezi kukosa kuitumia katika kutoa busu la kimahaba kwa mpenzi wake.

Alipoulizwa ni mara ngapi amebusu msichana, Morgan alisema kwamba anaweza hesabu ni mara ngapi lakini baadae akadai kwamba imefanyika mara kadhaa japo kwa msichana mmoja tu.

“Umewahi busu msichana?” Diana Marua alimuuliza Morgan.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

“Ndio! Angalia katika hii midomo mikubwa, ilitengenezwa ili kutotumika ipasavyo? Nimebusu ndio lakini sio katika hii shule, ni katika shule ya Juja.”

“Ukweli ni kwamba nimebusu na si mara moja, japo naweza hesabu ni mara ngapi…jambo zuri ni kwamba nimefanya mabusu kadhaa kwa msichana mmoja,” alisema.

Morgan Bahati//INSTAGRAM

Kijana huyo alieleza kwamba kabla ya kuondoka katika shule ya Juja mwishoni mwa 2023, yeye na mpenzi wake katika shule hiyo ambaye alibusu mara kadhaa walifanya maagano kwamba hakuna mmoja kati yao atakuwa na mpenzi mwingine licha ya wao kutokuwa pamoja tena.

“Wakati nilikuwa naondoka kule, tulikuwa tunafunga shule muhula wa 3 mwaka 2023. Tulifanya maagano kwamba hakuna atakayekuwa na mpenzi mwingine na tangu wakati huo mimi nimeheshimu makubaliano hayo kwani sijakuwa na mpenzi mwingine.”

“Japo nina namba yake ya simu, huwa hatuzungumzi na hata sijui kama alisonga mbele na maisha yake. Lakini hatumai bado. Nikigundua kwamba alipiga hatu kimaisha, nitahuzunika,” Morgan alijieleza.