Burunguti la pesa//MAKTABA

MHUDUMU wa teksi aliwashangaza watangazaji wa kipindi redioni alipopiga simu akitaka msaada wa kusaidiwa kumpata mteja wake aliyesahau kitita cha pesa katika gari lake.

Hii ilifichuliwa katika video inayovuma kwenye TikTok, ambapo kitendo cha nadra cha dereva kilipongezwa.

Kwa mujibu wa dereva huyo wa teksi, alimpa mteja huduma ya kumsafirsha hadi alikotaka na baada ya kushuka na kutokomea, aligundua mfuko wa mteja huo katika kiti cha nyuma.

Dereva huyo aliufungua mkoba ule na kwa kustaajabu alipata kitita cha dola laki moja – sawa na shilingi 12,995,000.

Akiwa amechanganyikiwa, dereva huyo alikwenda redioni kutaka kusaidiwa ujumbe wake kutangazwa ili kumfikia mteja wake, ambaye alihisi pengine pia alikuwa anataabika kuipata teksi ile aliyoabiri.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Hadithi hiyo ilipozidi kuvuma mtandaoni, watu wengi walifurika sehemu ya maoni ili kumpongeza dereva kwa uaminifu wake wa ajabu.

Wengine hata hivyo walimdhihaki kwa kile walihisi ni kuitupa baharini bahati yake na kudai kwamba huenda akaishi milele kuwa maskini.

×

Tazama baadhi ya maoni hapa chini:

@ezemalonginusuche: “mtu wa teksi atabaki kuwa maskini kwa vile hawezi kutumia nafasi ambayo Mungu amempa, mtu anayesahau dola 100,000 lazima apate dola 500,000 nyingine.”

@Daniel Ogbu Jr.: "Ni vipi mtu anavyoweza kushikilia $100k wakati yeye anatumia teksi... ikiwa yeye mwenyewe ni mwizi."

@Flexy: "Karibu kila mtu anamtukana huyu mtu. Hebu niambie mwanaume huyo atakuwa na amani ya akili kwa kufanya jambo sahihi. Nimefanya vivyo hivyo nilipokuwa kijana, begi lenye pesa."

@Enshi_Sheriff: "Ni kama vile utajiri huu wa kizazi unaanza, na mwizi mmoja mkubwa."

@Da Modest: “MUNGU anisamehe?? lakini dereva wa teksi hawezi kuwa tajiri tena maishani ️ikiwa Mungu anaweza kutumia samaki kusaidia mtu, bado uko huru kumwongoza baraka zake ??.”