
MKEWE mwinjilisti Guardian Angel, Esther Musila amewashauri watu kutotilia maanani sana kuchukiwa na binadamu wenzao, akitaja hiyo kuwa hali ya kawaida sana.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Musila alidai kwamba mtu kuchukiwa na watu ni kawaida na wala halifai kukuingia katika akili na kukupa Mawazo sana.
Ila alidai kwamba kama binadamu, unafaa kuwa na wasiwasi mkubwa ikiwa utaanza kuchukiwa hadi na Wanyama, haswa mbwa.
Kulingana na Musila, chuki kutoka kwa binadamu mwenzako ni kawaida sana kwani siku zote hasidi hana sababu lakini chuki kutoka kwa mbwa ni jambo la mashaka ambalo linakupasa kujiita mkutano na kujitathmini ulikobeta.
“Kama watu hawakupendi, si kawaida na sawa. Lakini Kamba mbwa hawakupendi, basi huo ni wakati wa kujiita mkutano na kujitathmini,” Musila alidai.
Lakini je, ni rahisi kupata mnyama aina ya mbwa kumchukia binadamu?
Kwa mujibu wa Rover.com, Mbwa hupenda wanadamu kutokana na mchanganyiko wa mambo, ikiwa ni pamoja na historia yao ya mabadiliko, akili ya kijamii, na uimarishaji mzuri wanaopokea kutokana na mwingiliano wa binadamu.
Mbwa wamefugwa kwa maelfu ya miaka, wakibadilika na kuunda vifungo vikali na wanadamu, na wana uwezo wa kuelewa na kukabiliana na hisia za kibinadamu na ishara za kijamii.
Wakati mbwa huingiliana na watu na kuwa na uzoefu mzuri, hupata kasi ya kujisikia vizuri ya dopamine, hivyo si rahisi kupata mbwa akimchukia binadamu.
Mbwa hupenda kulamba. Wakati mbwa anakulamba, anakubusu. Kumbusu ni ishara ya ulimwengu wote ya mapenzi, hata kati ya mbwa! Kulamba kwa mbwa pia ni tabia ya kutafuta umakini. Kwa hivyo ikiwa mbwa wako anakulamba, anaweza kuwa anakuuliza wakati wa kucheza, kubembeleza, au kipenzi.
Mbwa wako anapokujia na kuegemea uzani wake kamili dhidi ya miguu yako, anakuonyesha kwamba anakuamini na kukupenda kabisa.
Kwa maelezo haya, ni bayana kwamba si kawaida kwa mbwa kumchukia binadamu na ikitokea anamchukia, basi kuna suala kuu tena la dharura ambalo mtu unafaa kujiita mkutano.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!