Pasta Ezekiel

UNAAMBIWA watu mara nyingi hutafuta mwongozo wa kiroho, usaidizi wa kihisia, na usaidizi wa vitendo kutoka kwa wachungaji wanaowaaminia kuwatatulia hayo matatizo yao.


Wanaweza kuomba ushauri juu ya maamuzi ya maisha, mapambano ya kiroho, au kuhitaji tu mtu wa kusikiliza na kutoa uwepo wa kuunga mkono.


Sasa mzee mmoja amepeleka mizigo yake na kuishusha katika madhabahu ya kanisa la New Life prayer Centre linaloongozwa na mchungaji Ezekiel, akilalamika kuhusu vijana wake kukataa kuoa.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans


Kulingana na mzee huyo, vijana wake 2 wenye umri wa miaka 37 wamekataa kuondoka katika nyumba yake ili kuanzisha maisha yao kivyao, kwani muda wote wamekuwa waking’ang’ania kisengetua cha runinga na yeye sebuleni.


Mzee huyo alisema kwamba anahisi wanawe wamerogwa, kwani kwa muda wote amekaa nao, hajawahi waona au hata kuwasikia wakitongoza mwanamke.


“Mimi ni Mluhya kutoka Lugari, Sasa watoto wangu hawatongozi wasichana, wako tu kwa nyumba tunang’ang’ania remote. Hao vijana wangu wawili wako tu kwa nyumba, hawatafuti warembo na wako na umri wa miaka 37,” mzee huyo alieleza.


“Kazi yao ni ‘papa uko na remote’ na ni kwangu. Sasa nani aliniroga?” mzee huyo alihoji kwa uchungu.


Akionekana kumpa suluhisho, pasta Ezekiel alimwambia kwamba kuna mtu anayeishi kwenye Dari ya nyumba yake ambaye anawafanyia ushirikina vijana wake.


“Huyo mtu anafanya hivyo ikifika usiku vijana wako wanaota ndoto mara nyingi wakiwa na wanawake wa karoho, wakiamka hata akiongelesha msichana hawezi jibiwa sababu ameingiwa na roho ya kukataliwa katika ndoa. Hivyo anakasirika mpaka anaona hakuna haja ya kuzungumza na mrembo kwa sababu hakuna jibu chanya,” Ezekiel alimpa ufunuo.


×


Mzee huyo kwa upande wake alisisitiza kwamba amekuwa akiwashinikiza kuondoka kwake lakini majibu wanayompa ni mpaka wapate kazi nzuri ndio waondoke, kitu ambacho mchungaji Ezekiel alikitaja kama visingizio tu.


“Hivyo ni visingizio tu, kwani kuoa ni kama kikohozi, huwezi kizuia kikija,” Ezekiel aliongeza.


Lakini je, ni kweli kwamba kijana kuchelewa kuoa ni uwepo wa ushirikina katika maisha yake?