Harmonize

BOSI wa lebo ya muziki ya Konde Music Worldwide, Harmonize ameonyesha maendeoe ya jinsi anavyozidi kujiweka mbali na maisha ya nje, akisema kwamba lengo lake ni kuwa na kila huduma nyumbani kwake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Harmonize alichapisha video akionyesha kukamilika kwa chumba chake cha mazoezi ya kunyanyua vyuma ambacho kimeshehedi vifaa vyote vya gym.

Harmonize alisema kwamba katika orofa ya juu, ana studio kwa ajili ya kufanya kazi zake za muziki na chini ana gym hivyo itakuwa vigumu sana kwa watu kukutana naye nje.

Msanii huyo Alifichua kwamba itakuwa nadra sana kutangamana na watu nje ya jumba lake la Konde Village, akisema kwamba kitu pekee ambacho kitamfanya kutoka na anapoenda kutafuta matibabu kwani hospitali tu ndiyo hajaweka katika moja ya vyumba vyake.

Kwa mashabiki wake ambao wangependa kuchukua fursa muhali watakapomkuta, Harmonize aliwataka kufanya kumbukumbu njema naye ikitokea wamekutana nao nje, kwani kuonekana kwake kutakuwa kwa uchache wa ajabu.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

“Itakuwa ghali sana kuniona pale nje, hebu tutengeneze kumbukumbu nzuri ikitokea tumekutana kwa maana sasa nina karibia kila kitu ndani. Kitu pekee ambacho pengine sina kwa sasa ni hospitali,” Harmonize aliandika.

Msanii huyo alitoa angalizo zaidi kwa yeyote ambaye angependa kujiunga naye kwenye mazoezi katika gym yake ya nyumbani, akisisitiza kwamba watoto wa kike tu ndio watakaokubaliwa.

“Nimerahisisha kila kitu, Konde Fitness iko tayari nyumbani kwangu, na ningependa kuwa na waalikwa lakini wawe warembo pekee. Mnaona gym iko chini na studio iko juu, juu ya dunia. Tag warembo wale ambao wanapenda kushiriki mazoezi ya gym waambie gym ya baba iko tayari,” Harmonize aliongeza.