Sandra Dacha

MUIGIZAJI Sandra Dacha hatimaye amepata furaha baada ya akaunti yake ya Facebook yenye wafuasi takribani milioni moja kurejeshwa chini ya udhibiti wake.

Kupitia kwa akaunti mbadala, Dacha alitangaza kupata udhibiti kamili wa akaunti hiyo ambayo imekuwa mikononi mwa wadukuzi kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Dacha alikumbuka siku ambayo hiyo akaunti ilipodukuliwa mnamo Februari mwaka jana, alishindwa kulala na hata hamu yake ya kula ilipotea akabaki akilia bila msaada.

“Februari mwaka jana, ukurasa wangu wa Facebook ulidukuliwa. Na acheni niwaambie, maisha yangu hayajawahi kuwa sawa tena. Siku ambayo ilidukuliwa, nilishindwa kula, nilishindwa kulala, nililia, nikawika na kulia tena,” Sandra Dacha alisema.

Alishukuru usimamizi wa Facebook na rafiki yake Martin Githinji kwa kuwa wa msaada mkubwa kwake ambapo amekuwa akifuatilia mchakato wa kurejeshwa kwa akaunti hiyo mikononi mwake.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Alimtania Githinji kwamba kama si hali ya uchumi wa sasa, angempa zawadi ya Ndege aina ya helikopta.

“Lakini acheni niwaambie, baada ya panda-shuka zote, ninafuraha kutangaza kwamba akaunti hii imerudi kwangu, hallelujah. Shukrani zote ziende kwa Martin Githinji na timu ya Facebook.”

“Wewe Marto wewe aki ya Mungu kama sio huu uchumi ningekununulia chopper. Pole kwa kukusumbua katika muda wote huu,” Dacha aliongeza.

Akaunti hiyo ilidukuliwa ikiwa na wafuasi 962,000 mnamo Februari 2024 na kumuacha Dacha akiwa anategemea akaunti ya Kibinafsi kwenye ukurasa huo.