Marcus Rashford

GWIJI wa Manchester United, Wayne Rooney anahisi Man U inafaa kuhisi wasiwasi mkubwa baada ya kuona jinsi mchezaji wao Marcus Rashford anavyozidi kufana kwenye mkopo Aston Villa.


Hii ni baada ya kumtazama fowadi huyo akifanya vyema katika klabu ya Aston Villa Jumanne usiku, lakini akatambua jambo fulani kuhusu uamuzi wa mshambuliaji huyo kuondoka kwa mkopo.


Rashford alicheza zaidi ya saa moja dhidi ya Paris Saint-Germain, akitoa pasi nzuri ya Ezri Konsa, lakini Villa hawakuweza kurejea tena kwa muujiza.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans


Akiongea kwenye Amazon Prime baada ya mchezo huo, mchezaji mwenza wa zamani wa Rashford, Rooney alipendekeza Villa itahitaji kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao ikiwa wanataka kuongeza muda wa kusalia kwa fowadi huyo.


Hata hivyo, aliweka wazi kuwa upendeleo wake ulikuwa kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kurejea katika klabu yake kuu.


"Jambo kubwa kwao sasa ni kumaliza katika Ligi ya Mabingwa," Rooney alisema.


"Unawaona Asensio, Rashford kwa wao kuwabakisha wachezaji hao - na ninatumai hawatafanya hivyo.”


"Natumai Marcus Rashford atarejea Manchester United na kufanya kama alivyofanya usiku wa leo. Hilo ndilo jambo ambalo sote tunataka kuona kama mashabiki wa Manchester United. Lakini ili kuwabakisha wachezaji hao na kuwavutia wachezaji hao wa Ligi ya Mabingwa ni lazima wamalize kwenye Ligi ya Mabingwa, la sivyo hili litakuwa ni upotevu."


Mkongwe huyo alisema kwamba Rashford anaonekana mwenye uchu na ari ya kushinda mataji makubwa na Aston Villa, na kusema kuwa hiyo ni dalili mbaya kwa Man U ambao wanapitia kipindi kigumu baada ya kumtema kikosini.


"Na Marcus Rashford anahisi wazi ana nafasi nzuri zaidi ya kufanya vyema na kushinda mataji akiwa na Aston Villa.”


 


"Hiyo ni wasiwasi mkubwa kwa Manchester United, lakini kwa Aston Villa, hiyo ni ishara nzuri. Kwa mtazamo wa Marcus Rashford, nataka sana kumuona kama alivyokuwa usiku wa leo, akionyesha sifa zake zote."