Masauti//Instagram

MSANII Masauti kutokea Pwani ya Kenya kwa mara nyingine amezungumzia kisa kilichomsibu Mtwapa mwaka jana wakati akitumbuizia mashabiki wake.


Akizungumza katika mahojiano kwenye kituo kimoa cha redio humu nchini siku chache zilizopita, msanii huyo alirejelea kisa hicho ambapo alitupiwa nguo ya ndani na shabiki mwanamke wakati anatumbuiza kwenye jukwaa.


Masauti alikiri kwamba lilikuwa ni tukio la kustaajabisha na la kumpunga vile vile kwani hakuwahi fikiria angefanyiwa kitendo hicho na shabiki wa kike, akiitaja kama ishara ya mashabiki kumkubali kimuziki.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans


Katika kisa hicho kilichotokea mwaka jana, Masauti Alifichua kwamba baada ya kuidaka ile chupi, meneja wake alitaka akabidhiwe lakini Masauti akakwama nayo kabla ya kuinusa.


“Mwanzo Ilikuwa ni vibe nilikuwa niko shoo pale yatch watoto wa kike wakapagawa kumuona Masauti. Mtoto Fulani ambaye mimi sielewi anatokea wapi nashangaa ananirushia jichupi la pink. Nililidaka mwanzo nikashangaa duh!”


“Halafu meneja si unajua lazima amlinde msanii, hivyo aliniambia leta hapa, nikamwambia baba eh, hii nimetupiwa mimi, sasa wewe unataka nikupe kwa mpango gani? Nikamwambia tulia wacha nicheze nayo hii mpaka nimjue mwenye chupi ni nani,” Masauti alielezea tukio zima.


Masauti hata hivyo alisema kwamba baadae alikutana na mwenye kumrushia chupa na ‘kumalizana naye’.


“Chupi nilimrejeshea mwenyewe. Mwenye chupi tulimalizana,” Masauti alidakia.


Masauti akizungumzia tukio kwa mara ya kwanza mwaka jana, alisema kwamba hakuwa anatarajia hilo kwani kwa muda mrefu alikuwa anajua matukio hayo wanafanyiwa wasanii wa nchi za Magharibi na Ulaya.


“Nilirushiwa chupi, sijawahi kurushiwa chupi kwenye steji ila kwa mara ya kwanza nilirushiwa. Kwa yule ambaye alirusha bigup sana kwa sababu alinifanya nikajihisi vizuri, unajua video za kurushiwa chupi tushaziona kwa wasanii kina Drake sijui kina Burna Boy, halafu sasa mimi hapa Masauti pia nimekuwa msanii wa kwanza Mombasa kurushiwa chupi,” alisema.