
RAPA matata kutoka humu nchini, Khaligraph Jones ametangaza mpango wa kuwaleta mashabiki wake kindakindaki wasiopungua idadi ya 200 nyumbani kwake kuwatumbuizia moja kwa moja.
Hili ni wazo ambalo alilichapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram, ambapo alihisi kuchochewa na klipu ya rapa mmoja wa Marekani akitumbuizia kundi la marafiki na mashabiki wake nyumbani kwake.
Jones alisema kwamba baada ya kukamilisha mjengo wake mkubwa uliogonga vichwa vya habari kwa kukejeliwa kuwa na muonekano wa duka la jumla, atawaalika mashabiki kindakindaki 200 kuwapa burudani spesheli.
“Mashabiki 200 wale ambao ni kindakindaki kabisa wa OG kualikwa katika nyumba yangu kwa ajili ya hafla kama hii, fikira zenu ni zipi?” Jones alihoji.
Msanii huyo mara kwa mara amekuwa akiweka wazi kwamba vichocheo wake wakubwa katika muziki wa rap ni wanamuziki kutoka Marekani.
Akizungumzia jumba lake mapema mwaka huu lilipogonga vichwa vya habari za burudani, Jones alisema kwamba kwake ni sawa na kwa rapa tajiri, Rick Ross.
Msanii huyo alisema kuwa kwa jinsi ameboresha mazingira ya jumba hilo la kifahari, watu wanaokwenda kule watapata kuhisi uwepo kama ule wa boma la Rick Ross.
“Hamjazoea hizi settings, hapa ukikuja ni kama umeingia Amerika, kwa Rick Ross. Heshima ni lazima kwa OG,” Khaligraph Jones alisema huku akicheka.
Jones alishangazwa na watu ambao walikuwa wanachapisha picha na video za jumba lake mitandaoni wakiambatanisha na kauli za dharau kuhusu mjengo huo.
Hata hivyo, alionyesha kutoshtushwa na kauli hizo hasi akisema kwamba habari za kusemwa kuhusu mafanikio yake ndizo habari ambazo alikuwa akiomba kwa muda mrefu.
"Unaamka unapata unatrend sababu umejenga nyumba kubwa inakaa kama maduka, Mungu anajua haya ndio matatizo niliyokuwa natamani," Khaligraph alisema.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!