
SENETA wa kuteuliwa, Karen Nyamu amevutia maoni mseto mitandaoni baada ya kufanya video ya utani akiigiza kitendo cha mchungaji wa kanisa la Neno Evangelism, James Maina Ng’ang’a akivamia muumini kwa makofi kanisani.
Katika klipu hiyo ambayo imevutia maoni ya watu kwa wiki sasa, Ng’ang’a alionekana akimzaba makofi mepesi muumini wa kiume kwa kile alidai kwamba alimshtukia akiwa amesinzia wakati wa ibada.
Nyamu katika klipu yake ya maigizo, Alifichua kwamba kwa maoni yake hadhani kuna mtu anamchukia mchungaji huyo mwenye vimbwanga huku pia akimpa pole mzee aliyezabwa kofi.
“Ni mimi pekee ambaye ninampenda kamanda James Ng’ang’a? nafuu ya vichekesho baada ya nyingine, woi pole sana mzee wa kofia,” Karen Nyamu aliandika.
Katika video hiyo iliyoonekana kukera wengi wakiwemo hata wanasiasa, Ng’ang’a alimvamia mwanamume huyo kwa makofi kabla ya kumtaka kuondoka katika safu ya mbele na kuenda kuketi safu ya nyuma.
“Amka, toka hapa na kofia yako ya takataka. Toka hapa enda nyuma huko, mjinga!” Ng’ang’a alimfokea mwanamume huyo huku akimfuatisha kwa makofi 2.
Kisha akamgeukia yule mwanamke aliyekuwa ameketi kando ya yule mtu aliyelala, akiuliza kwa nini alimruhusu jirani yake alale. "Kwa nini unamruhusu alale?" Ng'ang'a alihoji.
Baada ya video hiyo, mbunge wa Homa Bay Town, Peter Kaluma alitoa maoni yake akitaka leseni ya kanisa lake kufutiliwa mbali kwa kile alidai ni kitendo cha kumvamia muumini.
"Hii ni mbaya sana! Kenya inahitaji kuwashtaki na kuwakomesha wahusika kama Ng'ang'a, na kufuta 'makanisa' kama Neno Evangelism, ambayo kiongozi wake anawanyanyasa waumini waziwazi, kabla hatujashuhudia mauaji mengine ya aina ya Shakahola," Kaluma alitoa maoni.
Ikumbukwe si mara ya kwanza kwa Ng'ang'a kukosolewa vikali kutokana na vitendo vyake vya kuudhi.
Mnano Februari mwaka huu, alizomewa kwa madai ya kumwaibisha mwanamke ambaye aliomba msaada wake wa kulipa kodi ya nyumba.
Mwenye nyumba wa Milka Moraa alikuwa amefunga nyumba yake baada ya kushindwa kuongeza karo. Akiwaza kuwa mchungaji wake angemsaidia, alikimbilia Ng’ang’a kutafuta njia ya kusonga mbele, lakini akakumbana na dhuluma na aibu baada ya pasta kumtaka atafute nyumba za bei nafuu ikiwa hangeweza kumudu karo.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!