
MJASIRIAMALI Esther Akothee ameonyesha kughafilika kwake baada ya mwanamke mmoja aliyemsaidia takribani wiki moja iliyopita kurudi kwake tena akihitaji msaada zaidi.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Akothee alichapisha ujumbe huo akisema kwamba siku 4 zilizopita, mwanamke huyo alimlilia kwamba hakuwa na mahali pa kulala baada ya kufungiwa nyumba.
Alimlilia msanii huyo ambaye kwa utu aliguswa na kumlipia kodi ya kila mwezi ya shilingi elfu 6.
Hata hivyo, kilichompandisha mori Akothee ni baada ya mwanamke huyo kurudi kwake tena safari hii akiwa na hitaji jipya la kutaka msaada wa hela za kununua chakula.
Ni suala lililoonekana kumkera Akothee ambaye alilichapisha kwenye Facebook yake na kuvutia maoni mseto, baadhi wakihisi mwanamke huyo aliyesaidiwa alikwenda hatua zaidi ya kuwa na mazoea.
“Unakumbuka yule mama fua nilimtumia 6k siku 4 zilizopita kumlipia malimbikizo ya nyumba yake? Alipiga simu jana kuomba pesa tena akisema anahitaji msaada wangu na hana hata 50 bob kumudu mahali pa kulala. "Boss ni mimi petronila, tafadhali mum, Leo sina magali pa Kulala, nitumie kitu kidogo nijisaidie1" Akothee alisema.
Katika hali ya kushangaza, Akothee Alifichua kwamba mwanamke huyo hata hakuweza kulipa kodi hiyo na kumtaja kama mama mwenye umri wa miambaye ni mvivu kupindukia.
“Hajawahi kulipa kodi alisema mwenye nyumba hakuwahi kupokea simu zake ?Kwa hivyo niliachana na vita kwa sababu nimeshindwa, yeye ni mvivu hata kutunza kwa muda mrefu, anaficha nguo chafu na huwa na haraka ya kuondoka, hawezi kupika wala kusafisha nyumba vizuri, hadithi zake zote hazijumuishi yeye ni marehemu 50s ? Mungu tafadhali, sitaki kuwa yeye nikua niache nibaki mitaani. Na hii uwomgo wa ujinga haha upate billionaire, huwezi kujenga punje inaishia hapo,” alisema.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!