
MCHEKESHAJI na mtengenezaji wa maudhui kupitia YouTube, Oga Obinna amevunja kimya chake baada ya safari yake kutoka kwa harusi ya kitamaduni ya msanii Prince Indah kukumbwa na kisa kisicho cha kawaida.
Obinna ambaye alitua katika sherehe hiyo katika kaunti ya Migori kwa kutumia helikopta alikuwa gumzo la mitandaoni baada ya jamaa mwenye umri wa makamo kurukia na kuning’inia Ndege hiyo wakati ilipokuwa inaondoka.
Katika video ambayo ilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii, kijana huyo alionekana kuwa na uchu wa kupaa angani pamoja na helikopta hiyo, na alifanikisha azma lake kwa kuirukia na kuruka nayo.
Obinna baadae alichapisha video hiyo na kusema kwamba kijana huyo angeanguka vibaya na pengine afe, watu wangemlaumu kwamba amemtoa kafara kwa ushirikina.
Hata hivyo, alisema kwamba rubani wao alionyesha utu alipoipaisha helikopta chini karibu na ardhi ili kumruhusu kijana huyo kutua kwenye shamba lililopo karibu na sherehe ilimoandaliwa.
“MIGORI KOMANDO??????.Sasa huyu angeumia wangesema tumemsacrifice ??♂️??♂️??♂️??♂️??♂️??♂️ Alikuwa na hamu ya kushikilia. Walinzi wakamuondoa, akarudi. Bahati nzuri alijining’iniza mwenyewe pembeni, ambapo mimi na mfanyibiashara Bruno tulikaa, tukamuona,pilot hakukuwa amemuona hata. Tulimshusha salama kwa shamba la wenyewe hapo mbele akarudi amebebwa kichampe,” Obinna alisema.
Tukio hilo la kushangaza liliongeza chachu katika suala zima la harusi ya kitamaduni ya msanii wa Ohangla, Prince Indah ambayo ilizungumziwa pakubwa Jumapili.
Harusi hiyo ya kifahari iliwaleta pamoja mabbwenyenye kutoka sekta mbalimbali ambapo kila mmoja alijitahidi kuonyesha mtindo wake wa kisasa katika fasheni.
Wengine kama Obinna walikwenda hatua zaidi kwa kukomboa Ndege aina ya helikopta na kutua nayo katika sherehe iliyojaa magari ya kifahari ya kila aina.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!