
MWANAMUME mwenye umri wa makamo amewazuzua watumizi wa mitandao wa TikTok baada ya kunaswa kwenye video akiwa katikati ya barabara na bango la kuomba msaada.
Kwa kawaida, watu wengi hujitokeza na mabango kwenye makutano ya barabara zenye shughuli nyingi yakiwa na jumbe za kuomba msaada kuhusu masuala kama matibabu, ufadhili wa elimu… lakini jamaa huyu alikuwa anaomba msaada ya kupewa gari.
Kilichowashangaza wengi, jamaa huyo alikiri kwamba alikuwa na kazi na gari lingemlrahisishia kazi yake.
“Mungu tafadhali gusa mtu yeyote wa kunibariki na gari kwa ajili ya kazi yangu,” Jamaa huyo aliandika kwenye bango lake akifuatisha na nambari ya simu.
Watu walitoa maoni mbalimbali, baadhi wakikashifu kile walichoita kutumia suala la omba-omba visivyo na kumtaka kuridhika na kazi kwani kunao wengi wasio hata na hiyo kazi na ndio wanastahili kusaidiwa.
Wengine pia walionekana kukinzana na dhana ya kumsaidia mtu maskini, wakisema kwamba mtu anasaidiwa na baadae kuwa jeuri kwani hakupitia ugumu kutajirika bali kupitia njia ya misaada.
Haya hapa ni baadhi ya maoni;
"Hakuna kitu kinachoumiza kama kuinua maskini ambaye siku moja atakumeza kabisa kwa sababu hawakukulazimisha kuwasaidia .....mimi Ama ... kamwe tena."
"Hakuna mtu anayepaswa kujaribu hii. kama mmiliki wa gari utajuta sana. Moja ya majuto yangu maishani ilikuwa kununua gari kwa mtu wa kufanya naye kazi." Mwingine alisema.
Eben alisema: "Nilichonifanyia rafiki yangu mwenyewe ????? nilikuwa nikifikiria nilikuwa nikimsaidia bila kujua kwamba alitaka kunipeleka kwenye kaburi langu la mapema ? hmmmmmm mimi kamwe hakuna mtu anayepaswa kujaribu kwamba utalia kama utafanya."
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!