Diana Marua, Bahati Kioko//Instagram

KEVIN Kioko maarufu kama Bahati ametangaza mpango wa kumnunulia mkewe, Diana Marua zawadi nyingine ya gari la kifahari.

Kupitia Instagram, Bahati alitoa maoni chini ya chapisho la Diana Marua ambaye alionyesha kuridhika na maisha anayopewa na mumewe kwa zawadi kochokocho.

Diana alionyesha gari aina ya Brabus ambalo Bahati alimpa wiki kadhaa zilizopita kama moja ya zawadi ya kusherehekea takribani muongo mmoja wa uhusiano wao.

“Diana Brabus, nitakuwa nadanganya kama nitasema maisha si mazuri,” Diana aliandika.

Akijibu, Bahati alisema kwamba gari hilo kwa vile limekuwa moja ya mada zilizozungumziwa sana katika mitandao ya kijamii, anapanga kumnunulia gari lingine la kifahari aina ya Lamborghini

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

“Hili gari limegonga vichwa vya habari sana, zawadi itakayofuata ni ya gari aina ya Lamborghini,” Bahati aliandika.

Mwishoni mwa Februari, Bahati alifanya kufuru ya karne kwa kumnunulia mkewe zawadi ya gari la pink la Brabus ambalo lilitajwa kuwa lenye thamani ya zaidi ya milioni 45 pesa za Kenya.

Gari hilo lilikuwa kelele cha jumla ya zawadi nane ambazo msanii huyo alimpa mkewe kama ishara ya kumshukuru na kumthamini kwa miaka 8 ya uhusiano wao ambapo wamebarikiwa na watoto 3.

Wawili hao walivalia mavazi ya waridi yaliyofanana, bila kujua kuwa mwanamuziki huyo alikuwa amenunua gari aina ya G-Wagon Brabus.

Bahati alifichua kuwa gari hilo lilikuwa na thamani ya KSh 45 milioni lilikuwa limeboreshwa kulingana na rangi ya waridi ya Diana.

Alianguka chini na kulia baada ya mumewe kufunua gari.