Alikiba//Instagram

ALIKIBA ametangaza tarehe rasmi ya tamasha lake la kuadhimisha miaka 20 ya safari yake kwenye mawimbi ya muziki.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Alikiba Alifichua kwamba tamasha hilo la kipekee litafanyika Aprili 19 visiwani Zanzibar ambapo makumi ya wasanii watakuwepo kutumbuizia mashabiki.

Akionyesha maandalizi ya tamasha hilo, Alikiba alichapisha moja ya video akifanya mazoezi na Live band, akisema kwamba mashabiki wataburudishwa moja kwa moja na wasanii usiku wote.

“Ninajiandaa kwa miaka 20 ya ALIKIBA. Je, uko tayari?” Alikiba aliuliza kupitia Instagram.

Baadhi ya wasanii ambao amethibitisha kuwaalika katika mkesha huo wa kusherehekea miaka 20 kwenye muziki ni pamoja na Darassa, Whozu, Chege Chigunda, Dulla Makabila miongoni mwa wengine.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Kuelekea siku yake kuu, msanii huyo amekuwa akizindua miradi mbalimbali ambayo amenukuliwa akisema kuwa ni katika mkondo huo wa kuadhimisha miaka 20.

Mwezi Machi mwaka jana, Alikiba alizindua kituo chake cha runinga, Crown Media kuadhimisha miaka 20.

Katika hafla iliyosheheni nyota wengi, Kiba alisema analenga kuwafikia watu wengi iwezekanavyo kupitia chombo chake kipya cha Crowns Media kitakachojumuisha kituo cha televisheni, redio, vyombo vya habari vya digitali na matukio mbalimbali.

Ali Kiba sasa anaungana na mwimbaji mwingine wa Tanzania Diamond, ambaye anamiliki jumba la habari kamili la Wasafi Media.

Diamond ni miongoni mwa waimbaji waliotamba sana nchini Tanzania na kwa hakika Afrika Mashariki, lakini kwa hakika ugomvi wake na Ali Kiba umewafanya wasambaratike zaidi.

Bila kujali, wote wawili wanafurahia mafanikio makubwa ndani na nje ya muziki.