Dkt. Mercy Mwangangi

Aliyekuwa katibu mwandamizi wa Afya Dkt. Mercy Mwangangi ameteuliwa afisa mkuu mtendaji mpya wa Mamlaka ya afya ya Jamii (SHA).

Kulingana na barua iliyotiwa saini na waziri wa Afya Aden Duale Mwangani ni mtaalamu wa masuala ya kifedha na sera za Afya. Ana tajiriba ya miaka 15 katika usimamizi wa afya ya jamii (UHC).

"Wizara ya Afya ingependa kutangaza uteuzi wa Dkt. Mercy Mwangangi kama Afisa Mkuu Mtendaji mpya wa Mamlaka ya Afya ya Kijamii," Duale alisema katika barua ya uteuzi.

Mamlaka hiyo haijakuwa na afisa mkuu mtendaji wa kudumu huku aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Elijah Wachira akitumwa kwa likizo ya lazima na bodi ya usimamizi kuruhusu uchunguzi wa utendakazi wake.

Uamuzi wa kumuondoa Wachira ulitolewa na Bodi ya Mamlaka hiyo, ikieleza haja ya uchunguzi wa kina kuhusu mienendo yake wakati wa uongozi wake.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

"Hii ni kukufahamisha juu ya Azimio la Bodi la kukutumia Likizo ya Lazima kuanza kutumika mara moja kwa muda wa siku Tisini (90) ili kuruhusu uchunguzi zaidi wa mienendo na utendaji wako wa kitaaluma kama Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Jamii," barua hiyo ilisema.

Robert Ingasira amekuwa akishikilia wadhifa huo.

“Wizara inampongeza Dk. Mwangangi kwa kuteuliwa na kumtakia kila la kheri kwani anakuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa kwanza wa Mamlaka ya Afya ya Jamii. Tuna imani kwamba anacho kinahitajika ili kuongoza SHA na kutekeleza majukumu ya SHA.”

Hadi kutueliwa kwake Mwangangi amekuwa akihudumu kama afisa mku wa mifumo katika shirika la AMREF Africa.

Dkt. Mwangangi anakumbukwa sana wakati janga la Covid 19 alipokuwa akitoa taarifa za kila wiki kuhusu hali ya maambukizi ya maradhi ya Covid 19 kwa taifa.