
MTANGAZAJI wa redio, Kamene Goro amezua mvutano kwenye mitandao ya kijamii baada ya kutoa ushauri ambao wengi wanauona kama wenye ukakasi kuhusu suala pana la uchumba.
Katika klipu fupi aliyoichapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram, Goro alishauri warembo haswa wale walioko katika umri wao wa miaka ya 20s kutumia ujana wao vizuri.
Mtangazaji huyo ambaye aliolewa miaka miwili iliyopita alishauri warembo katika miaka yao ya 20s kutumia ujana wao kufanya majaribio kwa wanaume kadhaa hadi pale watakapompata mmoja sahihi wa kutulia naye kwenye ndoa.
“Ninataka kuzungumza na warembo wangu walioko katika miaka ya 20s, ambao bado ni wadogo na ndio wanaanza kuona ni maana ya majukumu ya ukubwani, tafadhali, kwa njia yoyote usiwahi jifungia kwa mwanamume mmoja tu,” Goro alisema.
Kulingana naye, miaka ya mapema 20s ni ya kufanya majaribio ya kila aina kwani huu ndio umri ambao warembo wako katika ubora wao.
Goro alisema kwamba ni sahihi kujifungia kwa mwanamume mmoja tu ukiwa katika umri huo kwani ana uhakika kwa zaidi ya asilimia 1000 kwamba mwanamume wanayefikiri ni wao hawatamalizia katika ndoa naye, hivyo kuwataka kutanua wigo wao zaidi.
“Acha niwaambie kitu, ujana wao ni fursa yako ya kufanya majaribio, nendeni kule nje busu vyura wote hadi pale utakapompata wako akufaaye. Utajuaje mwenye anakufaa kama umekwama na mmoja tu?” Goro alihoji.
Aliwaasa warembo kufanya majaribio kwa wanaume wa kila aina kimuonekano, kitaaluma, kimaumbile na hata kwa rangi mbalimbali za Ngozi.
‘Enda uchumbiane na mtu ako na dread, chumbiana na mwanamume mweupe, mrefu...unajua,” Alijieleza.
Hata hivyo, alijua fika kwamba ushauri huu utamweka katika nafasi finyu miongoni mwa wafuasi wake katika mitandao ya kijamii lakini alisema kwamba ndiye mtu pekee mwenye ujasiri wa kuwaambia warembo ukweli ambao wengi hufichwa kuhusu uhalisia wa maisha haswa katika mabano ya umri alioutaja.
Kamene alifanya harusi ya faragha na mpenzi wake DJ Bonez miaka miwili iliyopita katika hali iliyowashangaza wengi ikizingatiwa kwamba alikuwa miongoni mwa warembo waliokuwa wakiona suala la ndoa kama lisilo na kipaumbele sana katika maisha ya mtoto wa kike.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!