Mwanamke afanya bonge la party

MWANAMKE mmoja mwenye umri wa makamo amezua gumzo katika mtandao wa TikTok baada ya kuandaa tafrija kubwa la kusherehekea kuweka rekodi ya kuwa mtu wa kwanza kutoka Kijiji chao kuairi ndege.

Katika video hiyo, mrembo huyo alibandika bango kubwa lenye ujumbe ‘mtu wa kwanza kutoka Kijiji chetu kupanda ndege’ kando ya viti na maturubai wakiwa wamefurika watu kujivinjari kwa sherehe.

Aliwaandalia mlo na kuwataka kujumuika naye kumsherehekea kwa kuweka rekodi hiyo adimu.

Tukio hilo liliwashangaza wengi, baadhi wakimhongera kwa rekodi hiyo na wengine wakimsuta kwa kuharibu hela katika kile walichokitaja kuwa jambo lisilo la maana.

Hata hivyo, wengi walionekana kukubaliana naye wakisema kuwa mtu anapoamua kusherehekea mafanikio yake japo madogo, aachwe tu asherehekee maana kwa wengine yanaweza yakaonekana ya kawaida tu lakini kwa mhusika ni makubwa na yenye thamani kubwa kwenye kumbukumbu ya maisha yake.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Tazama video hiyo hapa chini kisha utoe maoni yako;

×