Jinsi AFC Leopards ilitumia mapato kutoka kwa Mashemeji Derby

Klabu hiyo ilitoa taarifa kwamba ilikusanya zaidi ya shilingi milioni 7 na takribani thuluthi tatu zilienda katika kulipia madeni na huduma mbalimbali.

Walitumia shilingi 116,000 kulipia uwanja wa Nyayo Stadium huku shilingi 369,780 zikitumika kulipa waliotoa huduma za kuuza tikiti.

Aidha, shilingi 196,000 zilitumika kukidhi mahitaji ya timu kwenye kambi na shilingi 495,000 zikitumika kuhakikisha usalama uwanjani.