
MSANII maarufu wa miziki ya Bongo Fleva, Diamond Platnumz amedokeza kuchoshwa na gari lake la kifahari – Rolls Royce.
Kupitia Instagram stories zake, Diamond alichapisha picha ya gari hilo la kifahari lenye rangi ya samawati na kufuatisha na ujumbe kwamba amechoka kulitumia na sasa anajiandaa kupokea gari jingine la kifahari aina ya Bugatti.
Alidokeza kwamba Bugatti limo njiani linasafirishwa kutoka ughaibuni na pindi litakapofika, utakuwa mwisho wake wa kutumia Rolls Royce ambalo alinunua takribani miaka 5 iliyopita.
“Nimechoka na hii Rolls Royce, siwezi ngoja Bugatti langu kuwasili nyumbani,” Diamond aliandika.
Diamond alionyesha gari hilo kwa mara ya kwanza mwishoni mwa 2020 likiwa na nambari binafsi ya usajili yenye jina lake, Platnumz.
Baadae Julai 2021, alibadilisha nambari hiyo ya usajili na kuweka ‘SIMBA’ katika kile kilichoonekana kama ni kutimiza ndoto zake za muda mrefu.
Itakumbukwa Wakati fulani mwaka wa 2018 alisema katika mahojino kwamba angelinunua gari hilo ‘hivi karibuni’
Baada ya kulinunua, Diamond aliamsha popo kwenye Instagram baada ya kuweka kwenye bio yake kwamba ndiye mwanamuziki wa kwanza kutoka Afrika Mashariki kumiliki gari la Rolls Royce.
Mwaka wa 2016 nyota huo alionekana katika gari la jeupe la Rolls Royce lakini baadaye ikagunduliw akwamba alikuwa akifanya video ya wimbo wake
Gari kama hilo lenye gharama ya juu ni Rolls-Royce Phantom lilimgharimu kati ya $450,000 ( takriban shilingi 45,000,000) kipindi hicho.
Diamond anafahamika kwama mpenzi wa magari na wakati mwingi huyataja kama ‘my babies’
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!