
MWANZILISHI mwenza wa Microsoft, Bill Gates yuko kwenye orodha ya mabilionea ambao hawana mpango wa kuacha mali yao yote kwa watoto wao.
Watoto watatu wa Bill na mke wake wa zamani, Melinda Gates, watarithi kiasi kidogo cha utajiri wake.
Bado, hata sehemu ya utajiri wa Bill Gates ni zaidi ya dola bilioni. Mzee huyo mwenye umri wa miaka 69 hapo awali aliita "kosa" kutoa utajiri wake wote kwa watoto wake, akisema nyingi zitaenda kwa mashirika ya kihisani.
Thamani ya utajiri wa mkwasi huyo wa Microsoft inakadiriwa kuwa dola bilioni 155 (Shilingi za Kenya Trilioni 20.08) na Bloomberg Billionaires Index, lakini amesisitiza wanawe watafaidi 1% tu ya ukwasi huo.
Katika podcast na Raj Shamani, Bill Gates alisema kwamba ingawa watoto wake "walipata elimu na malezi bora", watapokea 1% tu ya utajiri wake.
Akishiriki jinsi chaguo zilizofanywa na familia tajiri kuhusu urithi wao kwa kiasi kikubwa zilitegemea maadili yao wenyewe, Gates, kwenye podikasti ya 'Figuring Out With Raj Shamani', alisema, "Kila mtu anaamua juu ya hilo."
Aliongeza kuwa watoto wake "walipata malezi na elimu kubwa, lakini chini ya 1% ya utajiri wote."
Bill Gates aliongeza kuwa hataki watoto wake "wachanganyikiwe kamwe kuhusu msaada wako kwao na upendo wako kwao".
"Sio nasaba, siwaombi waendeshe Microsoft. Nataka kuwapa nafasi ya kuwa na mapato yao na mafanikio," Gates alisema.
Bill Gates na Melinda French Gates wana watoto watatu kutoka kwa ndoa yao ya miaka 27. Mkubwa ni binti Jennifer (28), akifuatiwa na mtoto wa kiume Rory, 25, na binti wa miaka 22 Phoebe.
Kulingana na jarida la PEOPLE, Bill na Melinda walisitisha talaka yao hadi watoto wao wote walipohitimu shule ya upili. Wanandoa hao walitengana mnamo 2021.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!