Andrew Kibe//INSTAGRAM

MCHANGANUZI wa maswala mbalimbali ya kijamii mitandaoni, Andrew Kibe amedai kwamba kozi nyingi zinazotolewa katika vyuo vikuu kwa sasa hazina maana, ikizingatiwa ujio wa teknolojia ya AI.


Katika klipu moja aliyochapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram, Andrew Kibe alidai kwamba ujio wa AI umefanya kozi nyingi kuonekana zisizo na maana na kuwataka wanachuo ku’defer masomo yao na kurudi mitaani kuanzisha biashara.


Kibe alidai kwamba kozi pekee ambazo zimesalia kuwa za maana ambazo AI haitafanya kwa urahisi ni kama vile kozi ya udaktari na uhandisi.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans


Aliwataka wanachuo wanaofanya kozi zingine ambazo AI inaweza fanya kuokoa muda wao na kutafuta utajiri kwa kuachana na masomo hayo na kurudi mitaani kuanza ku’hustle.


“Kaka, kama uko chuoni, sitisha hiyo kozi unayofanya, rudi huku nje fungua biashara. Huo ni ushauri muhimu. Unafanya nini chuoni, pengine kama unafanya udaktari ama unataka kuwa mhandisi.”


“Hizi kozi zingine zote ni bure, hata hiyo ya fundi umeme unaenda kufanya nini? Enda kwa fundi atakufunza kila kitu unachohitaji kujua, kwa ground hakuna hiyo michakato mingi eti kuandika kwenye karatasi,” Kibe alishauri.


Andrew Kibe amekuwa akitoa ushauri ambao unawagawanya baadhi ya wafuasi wake mitandaoni, wengine wakihisi ni ushauri muhimu huku wengine wakimuona kama mtu mwenye lengo la kupotosha jamii.


Lakini je, ni ukweli kwamba teknolojia ya akili mnemba (AI) imekuja kuvuruga sekta ya uajiri kwa kuchukua majukumu mengi ambayo awali yalitegemea akili ya binadamu kutekelezwa?


Kwa mujibu wa Exploding Topics, Mwaka wa 2025 unaweza kuongeza kasi kwa mabadiliko makubwa ambayo AI tayari inasababisha kwenye soko la ajira.


Kadiri zana za AI zinavyozidi kuwa na nguvu, na kwa miundo ya LLM inayotarajiwa kama vile ChatGPT 5 na mawakala wa AI kama vile Manus ambayo ina uwezekano wa kuzinduliwa kwa matumizi ya jumla hivi karibuni, watu wengi zaidi wako katika hatari ya kuwa na kazi yao kufanywa kiotomatiki kikamilifu.


AI inaweza kuchukua nafasi ya kazi milioni 300 kote duniani. Hiyo inawakilisha 9.1% ya kazi zote ulimwenguni. Upotevu unaowezekana wa kazi hautasambazwa sawasawa katika sekta tofauti za uchumi. Badala yake, watakuwa wamejikita zaidi katika taaluma zilizo hatarini zaidi kwa kuwa otomatiki kupitia zana za AI za uzalishaji (kuandika, upigaji picha, ukuzaji wa programu, n.k.).