Kuvunjika moyo

MWANAMKE wa Kenya anayeitwa amezua gumzo kwenye mitandao ya kijamii baada ya kumkejeli aliyekuwa mume wake, ambaye alichukua mkopo kufadhili harusi yao ya kitamaduni.

Kulingana na mwanamke huyo aliyetalikiwa, mume wake wa zamani alitumia mkopo wa benki kulipia kila kitu wakati wa harusi yao ya kitamaduni ya kupendeza, lakini ndoa yao ilidumu kwa mwaka mmoja tu.

Akionekana kumfuma mkuki mume wake wa zamani kwa kile kilichoonekana kama uamuzi mbaya wa kifedha, alisema kwamba ndoa hiyo ilivunjika na mume huyo kubaki akilipia deni la mkopo.

Mke huyo ambaye alisema kwa madaha kwamba tayari ameshasonga mbele na maisha ya kupata mwenzi mpya, alimkejeli Ex wake kwa kubaki na deni la benki pamoja na riba lakini pia kuuguza moyo kutokana na ndoa kusambaratika.

“Kiwango [cha harusi] kilikuwa cha chini lakini mimi sikulipia hata senti kwa ruracio yangu. Yeye alilipia kila kitu kutoka kwa mavazi yangu, mapambo, mshereheshaji, video, chakula na hata vipodozi vyotealoigharamika yeye.”

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

“Ile shughuli ilikuwa ghali sana na sasa amebaki akilipia madeni peke yake wakati mimi niko vizuri katika maisha yangu ya kibiashara na pia nina mchumba mpya,” alisema.

caption

Mwanamke huyo alifuta chapisho lake baada ya kukosolewa vikali na watumiaji wa mitandao ya kijamii ambao walikutana na dhihaka zake dhidi ya mumewe wa zamani.

Waliokatishwa tamaa zaidi wamemwita mwanamke asiye na shukrani. Wamependekeza hata alikuwa akisaliti penzi la mumewe walipokuwa bado kwenye ndoa.