Msanii wa Kenya Stephen Otieno Adera alimaarufu Stivo Simple boy alijiachillia aliposema kuwa kuwa yuko Single.
Alisema kuwa aliamua kuwa Kapera kutokana na sababu nyingi za Wasichana kumtenda kinyume na mapenzi yake.
Alipozungumza akiwa katika mahojiano mnamo Ijumaa ya Machi 21,2025, mzawa huyo wa Kibra aliweza kusema kuwa baada ya kupitia mapigo kadhaa kimapenzi ya kukataliwa na wasichana aliowapenda aliamua kupiga hatua kimaisha na sasa hataki uhusiano.
Msanii Stevo simple boy anajulikana kutokana na ubunifu wake wa kuimba na kufanya mzaha kwa mashabiki wake ambao amekuwa akiwawacha vinywa wazi .
‘’Nilipigwa matukio sasa niko Single ,Wanadada walinikataa,sasa nikaamua mimi kama dragon,wacha tu niteme moto ‘’ Simple Boy alisema.
Maisha ya msanii stevo simple boy yamechochea sana maisha ya wakenya akiwapendeza kama msanii mchangamfu na mcheshi mkuu.
Ipo siku aliwahi kumtambulisha mrembo kwa jina Pritty Vishy kama mrembo wake kabla ya wao kuachana kwa muda wa miezi michache.Hatimaye aliweza kumtambulisha msichana mwingine kwa jina GRACE kama mchumba wake lakini baadaye waliwachana tena.
Siku za hivi karibuni aliweza kupigwa na m shutuko baada ya kukumbuka kuhusu zaidi ya mahusiano na wapenzi wake wa zamani ambapo walimdanganya zaidi ya mara 10 Jambo lililomfanya abadili Mawazo na kusema atafikiria masuala ya mapenzi mwaka wa 2026.
Simple boy aliweza kusema kuwa kuna vitu ambavyo yeye huvichukia kama kukosa uaminifu katika uhusiano akikariri kuwa jambo hilo huweza kuchangia pakubwa kuporomoka kwa mapenzi.
Stevo alisema kuwa aliyekuwa mpenzi wake wa zamani Grace aliweza kuzalishwa na mwanamume mwingine ilihali alikuwa na yeye bado katika mahusiano jambo ambalo lilimkata maini sana na kujihisi mnyonge wa mapenzi na mtoro kwa sasa.
Alisema kuwa hata baada ya Grace kujifungua mwana hakushughulika kutafuta babake mwana jambo ambalo lilimwacha akiwa amechanganyikiwa na kumwacha katika hali tete.
‘’Tulikuwa sawa hapo mbele tulikuwa tunaishi vizuri mke wangu alipokuwa karibu kujifungua mtu alinipigia simu na akaninong’onezea kuwa alihitaji kuniambia jambo aliniambia kuwa ulikuwa wakati mwafaka wa mimi kuambiwa ukweli na kuniambia kuwa nisikasirike, aliniambia mtoto si wangu hilo jambo lilinicha na mawazo makubwa.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!