
Rayvanny alikuwa akizungumza haya kwenye mahojiano na wanahabri huku pia akiisifia wasafi Kwa kuimushika mkono na pia kumusaidia msanii Mbosso.
"Kiukweli ni hivyo aliniuliza 'Mbosso' na tukashauriana. Nashukuru pia uongozi wa WCB wameweza kumuachilia bila kumulipisha chochote. Kwa hivyol sasa ana uhuru wa kuendelea kufanya kazi zake kibinafsi," alieleza.
Rayvanny pia ameenndelea na kusifia uwezo wa mwanamuziki Mbosso kwenye tasnia ya muziki akimutaja kama msani anayejituma na watu wanapenda sana uwezo wakie.
"Na ukizungumzia Mbosso ni msani ambaye anapendwa na watu wengi sana, Watu wanapenda sana uwezo wake," alisema Rayvanny.
Mwanamuziki huyo amempongeza Mbosso kwa kuamua kujipa changamoto mpya katika maisha hasa kwenye muziki. Ameeleza kwamba alimpa wasia Mbosso na kumueleza kwamba ajitume na asiogope kuanza safari ya kujitegemea kwani mwanzo mugumu lakini ndo kuianza safari.
"Nilimwambia, wale wale wanaokusifia ndio wale wale weatakaokusema, ila Mungu alisema unapoianza safari, kuna kutia moyo. unapoonyesha mafanikio vinaibuka vikwazo,' alieleza kwa kina.
Rayvanny aliamua kujiunga rasmi na moja ya lebo kubwa zaidi za kurekodi, WCB Wasafi mwaka 2015. Lebo hiyo ya Wasafi inasimamiwa chini ya uongozi wa msaniii Diamond Platnumz. Huko alitoa wimbo wake wa kwanza, "Kwetu", mwaka 2016. Na ulikuwa pigo katika Afrika Mashariki.
Baada ya safari ndefu ya miaka mitano Rayvanny aliondoka wasafi baada ya bosi wake Diamond Platnumz kumaliza uvumi huo kwa kuthibitisha kuondoka kwa mwimbaji huyo kutoka kwa lebo hiyo maarufu Oktoba 2020.
Mbosso alisainiwa na WCB Wasafi mwaka 2018. Na hapo ndipo ambapo alizindua tena kazi yake ya muziki kama msanii wa solo na kutoa nyimbo ikiwa ni pamoja na "Maajabu", "Picha Yake", "Tamu" na "Tamba"
Mnamo Januari 30, 2025, rafiki wa karibu wa Diamond, Baba Levo, alitangaza kuondoka kwa Mbosso kutoka Wasafi. Alisema kuwa msanii huyo ataruhusiwa kuondoka kwenye lebo bila mahitaji yoyote ya kifedha Kauli amboyo Diamond na Mbosso wote walitibithisha baadaye.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!