
MWANAMUME mwenye umri wa miaka 43 amehukumiwa kifungo cha miaka 14 jela baada ya kupatikana na kosa la kuvua mpira wa kinga bila ridhaa ya mrembo wake wakati wa kufanya mapenzi.
Mwanamume huyo aliyetambulishwa kwa jina moja tu la Lawrence katika mahakama moja jijini London, alikutana na mrembo, 32, katika programu ya uchumba mitandaoni mnamo Julai 2021 wakati safari yao ya mapenzi ilipoanza.
Baada ya kuchumbiana na kuzoeana kwa muda, wawili hao walikubaliana kukutana nyumbani kwa mrembo huyo na kukubaliana kufanya mapenzi, japo mrembo alisisitiza Lawrence kutumia kinga.
Mrembo huyo aliiambia mahakama kwamba aligundua wakati wa kujamiiana, Lawrence alivua kondomu kisiri na baada ya kumaliza tendo, Lawrence alimtaarifu kwamba alikuwa mwathirika wa virusi vya UKIMWI.
Dai la kuwa Lawrence alikuwa mwathirika wa virusi baadae lilipatikana kuwa uongo lakini alikutwa na hatia ya kumpa usumbufu wa kiakili mrembo kwa kumdanganya.
Pia, Lawrence aligundulika kuwa alitumia anwani ya uongo na taarifa ya benki, na pia kutumia simu ya kulipia kabla ili kujaribu kuzuia kugunduliwa na polisi.
Pia alidai kuishi katika nyumba ya mamilioni ya pauni, lakini ukweli alikuwa akiishi katika ghorofa ya kawaida, Maelezo hayo yalisomeka kwa mujibu wa London Evening Standard.
Baraza la mahakama lilimpata na hatia ya kubaka mnamo Oktoba, na pia alikiri kosa la kumnyanyasa mwathiriwa.
Mnamo Februari 2022 alikiri hatia ya mawasiliano mabaya na vitisho vya kufichua picha ya kibinafsi kwa waathiriwa wawili tofauti.
Lawrence pia alikuwa ametumia jina la uwongo na alikutana na mwanamke huyo mtandaoni, na akawatisha baada ya kukutana nao.
Kufuatia hukumu yake, Inspekta Mkuu wa Upelelezi jijini London alisema: "Ningependa kumpongeza mtu huyu aliyenusurika kwa ushujaa alioonyesha katika kesi hii na ushahidi aliotoa.”
"Hukumu kali iliyotolewa na hakimu inaonyesha wazi hatari kubwa ambayo mwanamume huyu analeta kwa wanawake.
"Timu ya uchunguzi ilifanya uchunguzi wa kina, wa bidii na usio na huruma ili kubaini Lawrence na kupata ushahidi wa kumfikisha mahakamani kuhakikisha kuwa mwathiriwa aliungwa mkono kote.”
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!