
FAUSTINE Lipuku Lukale, mpiga picha ambaye aliibuka kuwa rafiki wa kipekee aliyesimama na familia ya TikToker Brian Chira wakati wa kifo chake amefunguka yale aliyojifunza wakati na baada ya kifo hicho.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Lukale ambaye wengi wanamfahamu kama Baba Talisha aliungana na mamia ya mashabiki wengine wa marehemu Brian Chira kuadhimisha kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu kufa kwake katika ajali.
Alisema kwamba tangu kifo cha rafiki huyo, amejifunza mambo mawili makuu, yote yakionekana kurejelea mishale aliyotupiwa baada ya kusimama na familia yake katika mazishi.
Baba Talisha ambaye aliburuzana na nyanyake Brian Chira siku chache tu baada ya kuongoza TikTokers wenzake kuchangisha zaidi ya shilingi milioni 8 kwa ajili ya mazishi ya Chira, alisema kwamba hajutii hata kidogo fadhila alizoonyesha.
“Mwaka umepita na Leo inanikumbusha mambo 2 tangu Huyu Kijana Chira aondoke.
1. Usijutie fadhili ulizoonyesha mtu ambaye hakustahili. Walikukosea, ukawatendea mema, na kwa ajili hiyo unapaswa kujivuna.
2. Siku moja, mtu uliyejitolea sana kwa ajili yake atageuka na kusema hakuwahi kuomba, na itaumiza kwa sababu watakuwa sahihi,” Baba Talisha alisema.
Brian Chira aliaga dunia Machi 16 mwaka uliopita katika kile kilichoripotiwa na polisi kama ajali ya kugongwa na gari barabarani.
Jumamosi, TikToker mwenzake ambaye mpaka sasa amesalia kuwa msaada wa pekee kwa nyanyake Brian Chira, Obidan Dela alitembelea familia hiyo na kurekodi video wakiadhimisha mwaka mmoja tangu kifo cha mpenzwa wao.
Katika video hiyo, Obidan Dela na Watoto hao walikuwa wameishikilia picha kubwa ya Brian Chira huku wakikumbuka na kukariri kauli aliyopenda kuitamka ‘kama wewe si pesa huwezi nipa stress’.
Pia waliimba kwa huzuni wimbo wa Otile Brown ‘One Call’ ambao ulisheheni sana wakati wa mazishi ya Chira ambapo ilisemekana ulikuwa moja ya nyimbo alizozipenda pakubwa.
“Yo guys, Obidan Dela hapa, guys, na niko na Brian Chira na Sophie Njeri Chira Kadogo na wananiambia kama vile Chira alikuwa anawaambia, ‘Kama wewe si pesa, huwezi ni-stress.’”
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!