Safari na Usuli wa wasanii Radio and Weasel
Radio and Weasel lilikuwa ni kundi la wanamziki wawili kutoka taifa la Uganda walioimba miziki chini ya Bendi maarufu ‘’Goodlyfe Crew’’
Msanii Moses Nakintije Sekibogo alimaarufu(Radio) na mwenzake Douglas Mayanja alimaarufu( Weasel) ni wasanii waliotamba na kuvuma sana miaka ya hapo awali ya 2008-2018
Msanii Radio alikuwa maarufu na mpevu wa kuimba muziki aina ya RnB ilihali Weasel Naye akitia na kuongezea utamu wake wa aina ya muziki wa Reggae Ragga iliyokuwa na msisimko wa kucheza na kukatika katika mtindo wake wa kipekee.
Moses Radio alianza tasinia yake ya mziki akiwa shule ya upili kwanzia mwaka wa 1998 -2001 katika shule upili ya msalaba mtakatifu iliyoko Jinja ambapo kwa wakati huo pia alikuwa kiranja mkuu katika shule hiyo , akiwa shuleni aliweza kujiunga na klabu ya mashindano kwa Vijana ya mziki.
Akiwa pale shuleni Radio aliweza kukadiria mradi wa kubuni mradi kuhusu mziki ambapo ulielezea wazi faida za vipaji katika ulingo wa sanaa ya mziki kwa ujumla wasilisho lake hilo liliweza kushinda katika siku ya mashindano.
Hatimaye Radio alijiunga na Chuo kikuu cha Kiira ambapo aliendeleza kipaji chake kwa miaka miwili hatimaya aliazimia kujiunga na kundi la msaniii maarufu Jose Chameleon akiwa anamfanyia kazi nguli huyo Jose Chameleon kama mtu wake wa mkono aliweza kupewa fursa ya kuonyesha makali ya kipaji chake.
Aliweza kucharaza vibao kama Jenniffer, Dagala, Wololo, na kibao chake Sweet Lady kibao ambacho kiliweza kuvuma na kupokelewa na mashabiki wake na kumtukuza na kumsifu kama msanii mchanga ambaye alikuwa amekuja kwa moto kama wa kivu.
Kwa upande mwingine Douglas Mayanja alimarufu Weasel alianza kama msanii wa kujitegemea aliyekuwa akiimba kama msanii wa kujitegemea chini ya ulezi wa ndugu yake mkubwa, hatimaye Weasel alipata fursa ya kuimba kolabo kali sana na msanii Jose chameone na wakacharaza kibao kimoja kiitwacho ‘’ BOMBOCLAT’’ kibao ambacho kilivuma sana.
Baadhi ya vibao ambavyo wasanii hawa waliweza kuvicharaza ni kama Nakudata mwaka wa 2008,Lwaki Onumya,Zuena,Nyambura na kibao cha Bread and Butter.
Wasanii hawa waliweza kupokea zawadi nyingi katika taasinia yao hio ya muziki na kupata tuzo kibao kama tuzo ya Mziki wa HIPpop 2015,Hipipo wimbo bora wa mwaka 2015, Peal African music Award wimbo bora wa mwaka Nakudata 2008 miongoni mwa tuzo nyingine nyingi.
Mnamo mwaka wa 2018 msanii Radio Aliaga dunia kutokana na majeraha ya akili baada ya kupigwa na mlinzi wa usalama katika klabu moja kule Entebee alipokuwa akiwasilisha na kuimba katika klabu na kutupwa mita tatu kutoka juu na kurushwa chini sakafuni ambapo alipata majeraha kadhaa yaliomsababishia mauti yake.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!